FM Manyara

So They Can Tanzania lanufaisha matibabu wananchi 1,500 Manyara

6 September 2024, 5:32 pm

Kutokana na uhitaji mkubwa wa matibu halmashauri ya Babati inatarajia kushirikiana zaidi na mashirika mbali mbali yanayotoa huduma za afya kufanya kambi kwa kila robo ya mwaka ili kuwafikia wenye changamoto mbalimbali za afya kwenye maeneo yao katika halmashauri hiyo.

Na Marino Kawishe

Zaidi ya wananchi elfu moja na mia tano kutoka kata za Galapo, Qash, Endakiso na Mamire zilizopo halmashauri ya wilaya ya Babati mkoani Manyara wamepatiwa huduma mbali mbali za matibabu  kwenye kambi  ya matibabu ya  siku tano iliyoanza siku ya September 2 hadi September 6.

Akizungumza na Fm Manyara radio meneja mkazi wa shirika la so they can Tanzania  (stc) Roselyine mariki  amesema lengo  la kambi hiyo ya mtibabu nikuwafikia wananchi ambao wengi wao hawana uwezo wakufika hospital  na kwenye vituo vya kutolea huduma  za afya kwa sababu mbali mbali.

Sauti ya meneja mkazi wa shirika la So they can Tanzania  (STC)

 kwa upande wake Mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Babati Madama Hosea amesema kuna uhitaji mkubwa wa matibabu kwa wananchi hasa ambao wapo pembezoni na vituo vya afya nakusema wanafikiria kushirikiana zaidi na mashirika mbali mbali yanayotoa huduma za afya kufanya kambi kwa kila robo ya mwaka ili kuwafikia wenye changamoto mbali mbali za afya kwenye maeneo yao katika halmashauri hiyo.

Sauti ya Mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Babati

Aidha, huduma zilizotolewa  na madaktari katika  kambi hiyo  ya matibabu ya afya iliyoratibiwa na shirika la so they can  Tanzania (stc) kwa kushirikiana na halmashauri ya wilaya ya Babati na wadau wengine wa afya ni pamoja na ushauri wa lishe  kwa wananchi na watoto, vipimo na matibabu kwa magonjwa ya kinywa na meno, masikio, macho, upimaji wa vvu-ukimwi, uchangiaji damu na elimu kuhusu bima ya afya pamoja na magonjwa yasiyoyakuambukiza ikiwemo presha na sukari.