FM Manyara

Zaidi ya watoto elfu kumi wenye miguu kifundo wapatiwa matibabu

2 September 2024, 5:49 pm

Kambi ya siku tano ya matibabu imeanza leo katika  kata za Galapo na Qash kwa ufadhili wa shirika la So they can, kwa kutibu magonjwa mbali mbali ikiwemp kutibu watoto wenye changamoto ya miguu kifundo.

Na Marino Kawishe

 Zaidi ya watoto elfu kumi kuanzia umri wa  siku sifuri hadi miaka kumi na nane hapa nchini  wenye ulemavu wa waviungo ikiwemo miguu kifundo pamoja na midomo wazi wamepatiwa matibabu na shirika lisilo la kiserikali la Kafika house lenye makao makuu mkoani Arusha.

Akizungumza na fm Manyara, kwenye kambi ya siku tano ya matibabu kwenye halmashauri ya wilaya ya Babati iliyoanza leo kwa kata za Galapo na Qash kwa ufadhili wa shirika la So they can, meneja wa huduma mkoba kutoka shirika la Kafika house Rehema Simon ameelezea aina za ulemavu ambao watoto huzaliwa nao na ambao wamekuwa wakipambana nao  katika utoaji wa matibabu.

sauti ya meneja wa huduma mkoba kutoka shirika la Kafika house Rehema Simon

Aidha,amesema changamoto kubwa iliyopo kwa jamii ni kukosa elimu sahihi  ya ulemavu ambao unaweza kutibika,kutokana na baadhi ya mila kuhusika kuficha watoto hao ndani na kutowapeleka shule.