FM Manyara

Ajali yauwa wanne Manyara

August 31, 2024, 7:21 pm

Wanafunzi watatu na dereva mmoja wamefariki katika ajali iliyotokea wilayani Babati mkoani Manyara.

Na Mzidalfa Zaid

Watu wanne wamepoteza maisha wakiwemo Wanafunzi watatu na Dereva mmoja katika ajali iliyohusisha Coaster na gari la mizigo aina ya Scania katika eneo la Gajal wilayani Babati Mkoani Manyara ambapo Coaster ilikuwa imebeba Wanafunzi kutoka Hanang kuelekea Mkoani Arusha na baada ya Kufika eneo hilo iligongana uso kwa uso na Scania.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Manyara Ahmed Makarani amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo , amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa Dereva wa lori kushindwa kuwa makini barabarani na kuigonga Coaster hiyo iliyokuwa imebeba Wanafunzi 33 wa Shule ya Sekondari Endasaki waliokuwa wakielekea Mkoani Arusha kwa ajili ya likizo .

sauti ya Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Manyara Ahmed Makarani

Nao baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo, wamesema mteremko uliopo eneo hilo unapelekea kuwepo kwa ajali nyingi, ambapo wamewaomba waendesha vyombo vya moto kuendesha taratibu wanapofika kwenye mteremko huo.

sauti ya ya mashuhuda