FM Manyara

Jeshi latoa tuzo Kwa bilionea Mulokozi

August 31, 2024, 7:16 pm

Taasisi ya kijeshi ya command and staff college imetoa tuzo kwa Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Mati super brands ltd David Mulokozi kutokana mchango mkubwa aliounyesha katika taasisi hiyo.

Na Mzidalfa Zaid

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Mati super brands ltd David Damian Mulokozi amepokea tuzo maalum  kutoka taasisi ya kijeshi command and staff college kwa kile kilichotajwa kuwa mchango wake mkubwa katika mafunzo ya maofisa wa jeshi kutoka nchi mbalimbali waliyoyapata kupitia ziara maalumu ya kimafunzo katika kampuni ya Mati super brands ltd. 

Akiongea baada ya kupokea tuzo hiyo, Mulokozi amesema ni tuzo kubwa ambayo ameipokea na imewapa nguvu ya kuendelea kufanya kazi nyingi zinazoigusa jamii kwa ujumla.

sauti ya Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Mati super brands ltd David Damian Mulokozi

Tuzo hiyo adhimu ambayo hutolewa mara chache kwa watu na kusudi maalumu, imekabidhiwa na colonel verus chrysostom mbuzi kwa niaba ya mkuu wa chuo cha command and staff college, brigedia general sj mkunde comdt, ambapo inatambua juhudi na ufanisi wa. mulokozi katika kutoa maarifa, kujituma, uzalendo, ujasiri, uaminifu, na uadilifu katika mafunzo hayo.

mbali na mchango huo katika sekta ya mafunzo ya kijeshi, david mulokozi ametambuliwa kwa jitihada zake katika kuunda na kudumisha mazingira bora na salama ya uzalishaji kupitia kiwanda cha mati super brands ambapo viongozi wa kijeshi waliotembelea kiwanda hicho wameridhishwa na usalama wa chakula na usafi wa maeneo ya uzalishaji.

 licha ya kuwa kielelezo cha uongozi bora wa david mulokozi tuzo hii pia inafunguaa njia kwa wawekezaji wengine hasa katika sekta ya uzalishaji kutoa mafunzo, na kuonyesha namna ambavyo maarifa na maadili vinaweza kuunganishwa kwa manufaa ya jamii na taifa kwa ujumla.