FM Manyara

Mwigulu asema serikali inaboresha mazingira bora ya elimu

22 August 2024, 4:37 pm

Waziri wa fedha na mipango Mwigulu Nchemba ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa chuo cha uhasibu Arusha kamapasi ya Babati

Na Mzidalfa Zaid

Waziri wa fedha na mipango Mwigulu Nchemba  amesema uwepo wa chuo cha uhasibu Arusha kampasi ya Babati kitasaidia wananchi kutoka maeneo mbali mbali kupata elimu bora katika chuo hicho kutokana na namna serikali ilivyoboresha mazingira bora ya mwanachuo kujisomea.

Amesema hayo leo akiwa mkoani Manyara katika hafla fupi ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa chuo cha uhasibu Arusha kamapasi ya Babati ambapo amesema chuo hicho kitaongeza maarifa, ubunifu na kukabiliana na changamoto nyingine za kiuchumi.

sauti ya Waziri wa fedha na mipango Mwigulu Nchemba

Kwa upande wake mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha profesa Eliaman Sedoyeka amesema wataandaa mitaala ambayo inaendana na uhitaji wa soko na mategemeo ya wananchi wa mkoa wa Manyara ambapo kwa mwaka wa masomo 2023/2024 kutakuwa na kozi 72.

sauti ya mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha profesa Eliaman Sedoyek

Aidha, mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga, amesema uwepo wa kampasi hii kutasaidia ukuaji wa uchumi kwa mkoa wa manyara kwa kuwa wageni watakuwa wengi na wafanyabiashara watanufaika kwa kuuza vitu mbalimbali kwa wageni .

sauti ya mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga