FM Manyara

DC Twange: Kiwanda cha Dachkona kimeongeza ajira kwa vijana

9 August 2024, 6:11 pm

Kutokana na changamoto za ajira kwa vijana nchini, kiwanda cha Dachkona Company Ltd kinachotengeneza vinywaji mkoani Manyara kimeisaidia serikali kupunguza changamoto ya vijana kuzagaa mtaani bila ajira.

Mkuu wa Wilaya ya Babati mkoani Manyara Lazaro Jacobo Twange, amekipongeza kiwanda cha Dachkona Company Ltd kinachotengeneza vinywaji chagamshi kwa kuajiri vijana pamoja na kuongeza uchumi mkoani hapa kutokana na uzalishaji wa vinywaji kwenye kiwanda chake.

Akiongea baada ya kuzindua tamasha la michezo la jogoo lililofanyika katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa Stadium, Twange amesema kiwanda hicho kimeisaidia serikali kupunguza changamoto ya vijana kuzagaa mtaani bila ajira.

Sauti ya DC Twange

Kwa upande wake meneja wa kiwanda hicho  Nobert John, amesema lengo la kuandaa tamasha hilo ni kushirkiana na jamii ya mkoa wa Manyara katika shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwashukuru wateja wao ambao wamekuwa wakinunua bidhaa zao.

Sauti ya meneja wa kiwanda  Nobert John

Aidha, baadhi ya washiriki wa tamasha hilo wameushukuru uongozi wa kiwanda hicho kwa kuwa tamasha hilo limewasaidia kufanya mazoezi ya mwili na kupunguza magonjwa mbalimbali.

Sauti ya washiriki wa michezo.