Wafanyabiashara Manyara watakiwa kutumia EFD mashine
6 August 2024, 6:51 pm
Imeelezwa kuwa lengo la kuanzishwa kwa mfumo wa mashine za kieletroniki (EDF) mashine ni pamoja na kumrahisishia mfanyabiashara utunzaji wa kumbukumbu za biashara kwasiku
Na marino kawishe
Wafanyabiashara mkoani Manyara wametakiwa kuendelea kutumia mashine za Kieletroniki(EFD)kwenye biashara zao ili kuondoa usumbufu wakati wa ukadiriaji wa kodi na kupunguza malalamiko yanayoweza kutokea wakati wa ukadiriaji wakodi ya mapato.
Meneja wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA mkoa wa Manyara Joshua Mille ameyasema hayo alipokuwa akizungumza katika kipindi cha Trafick light kinachorushwa na kituo cha Fm Manyara radio,amesema lengo la kuanzishwa kwa mfumo huo wa mashine za kieletroniki (EDF) mashine ni pamoja na kumrahisishia mfanyabiashara utunzaji wa kumbukumbu za biashara kwasiku.
kwa upande wake kaimu afisa elimu ya mlipa kodi TRA mkoa wa Manyara Ephraim Medad amesema msambazaji anawajibu wa kuuza, kuwafungia na kuwafundisha matumizi sahihi ya mashine ambapo wafanyabiashara wanatakiwa kuwa na mashine hizo.
Aidha,utaratibu wa kutumia mashine za kielectroniki (EFD) ulianzishwa rasmi mwaka 2010 kwa wafanyabiashara waliosajiliwa katika kodi ya ongezeko la thamani vat kwa utekelezaji wa sheria ndogo ya efd ya mwaka 2010.