FM Manyara

Wananchi Manyara epukeni vishoka wa umeme

August 6, 2024, 5:44 pm

picha ya afisa mahusiano na mawasiliano kutoka mamlaka ya udhibiti wa huduma  za nishati na maji(Ewura)

Mamlaka ya udhibiti wa huduma  za nishati na maji(Ewura) imewataka wananchi mkoani Manyara kuepuka vishoka ambao wamekuwa wakifanya kazi na kusababisha madhara makubwa kwenye mifumo ya umeme

Na Mzidalfa Zaid

Wananchi  mkoani  Manyara na kanda ya kaskazini kwa ujumla  wametakiwa kutumia mafundi umeme ambao wamesajiliwa na wanye leseni Ili kuepuka vishoka ambao wamekuwa wakifanya kazi na kusababisha madhara makubwa kwenye mifumo ya umeme.

Wito huo umetolewa  leo na afisa mahusiano na mawasiliano kutoka mamlaka ya udhibiti wa huduma  za nishati na maji(Ewura)  Pamela Pallangyo alipokuwa akiongea na Fm Manyara amesema kuna baadhi ya mafundi umeme wanafanya kazi bila leseni.

Pallangyo amewataka wananchi kufika kwenye ofisi za Ewura pindi wanapohitaji ufafanuzi  au wanapokutana na changamoto kuhusu sekta ya maji, umeme na gesi ili malalamiko yao yatatuliwe kwa urahisi..

sauti ya afisa mahusiano na mawasiliano kutoka mamlaka ya udhibiti wa huduma  za nishati na maji(Ewura)

Aidha, amesema kwa fundi yeyote ambae anahitaji kupata leseni afatilie kwenye mamlaka hiyo ili apatiwe leseni na afanye kazi kwa uhuru ili kuepuka kuchukuliwa hatua za kisheria na mamlaka husika.