FM Manyara

 Vijana Manyara changamkieni fursa

July 29, 2024, 6:02 pm

picha ya mkuu wa chuo veta Manyara

Vijana mkoani Manyara wametakiwa kuchangamkia fursa zinazotolewa na serikali ili kujiendeleza kielimu hususani katika vyuo vya ufundi ili  kujiajiri na sio kusubiri kuajiriwa.

Na Mzidalfa Zaid

Mkuu wa chuo cha veta Manyara Nasanga Masange ameyasema hayo alipokuwa akiongea na Fm Manyara,amesema chuo hicho kimewasaidia vijana wengi kujiajiri kwa kupata elimu ya fani mbali mbali.

Amesema vijana wengi ambao wamepitia chuoni hapo wameajiriwa kwenye kampuni mbalimbali na wengine kujiajiri wenyewe ambapo amewataka wazazi kuwapeleka watoto wao kwenye vyuo vya ufundi ili watimize ndoto zao.

sauti ya mkuu wa chuo veta Manyara