Manyara yajipanga kukuza uwezo wa wafanyabiashara
24 July 2024, 5:37 pm
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga amesema baada ya maonesho ya wafanyabiasha sabasaba yaliyofanyika jijini Dar es salaam nakuwakutanisha wafanyabiashara kinamama na taasisi inayojishughulisha na wakina mama wanaosafirisha bidhaa nje ya nchi wanatarajia kufanya mkutano na kinamama wazalishaji na wasafirishaji ili kujadili fursa mbali mbali na kusafirisha bidhaa nje.
Na George Agustino
Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga amesema mkoa umejipanga kukuza uwezo wa wafanyabiashara wa ndani ya mkoa wa Manyara kwa kuwatoa na kuwashirikisha katika maonesho mbalimbali ya kibiashara ya nje na ndani ya mkoa watakayoanza kuyaandaa.
Sendiga ameyasema hayo leo julay 24 2024 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, amesema katika maonesho ya wafanyabiashara sabasaba yaliyofanyika jijini Dar es salaam kitaifa kwa mwaka 2024 mkoa wa Manyara umeshiriki na wafanya biashara wa ndani ya mkoa walioshiriki ambapo wamepata manufaa makubwa kwa kutangaza na kuuza bidhaa zao pamoja na kupata masoko ya nje ya nchi .
Aidha Sendiga amesema kupitia maonesho hayo ya sabasaba wamewaunganisha wafanyabiashara kinamama na taasisi inayojishughulisha na wakina mama wanaosafirisha bidhaa nje ya nchi ambapo wanatarajia kufanya mkutano na kinamama wazalishaji na wasafirishaji ili kujadili fursa hizo za kusafirisha bidhaa nje.