FM Manyara

Nkigi: Abiria acheni uoga

July 18, 2024, 11:35 am

Picha ya Mwenyekiti wa Chama cha Kutetea Abiria Tanzania (TAKUHA) Solomoni Nkigi

Abiria mkoani Manyara wametakiwa kupaza sauti zao na kutokuwa waoga wanapoona kuna changamoto katika vyombo vya usafiri kama dereva kukimbiza gari kwa kutoa taarifa katika vyombo vya sheria ikiwemo jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani pamoja na chama cha kutetea abiria nchini  (TAKUHA) ili kupatiwa msaada.

Na, Hawa Rashidi

Wananchi wilayani Babati mkoani Manyara wametakiwa kuzifahamu haki zao za msingi wanapokuwa katika vyombo vya usafiri kama abiria kwakua zitawasaidia wanapokutana na  changamoto katika vyombo hivyo vya usafiri.

Mwenyekiti wa Chama cha kutetea abiria nchini (TAKUHA) Solomoni Nkigi ameyasema hayo julay 17 alipokuwa akiongea na Fm Manyara, amesema abira wengi hawazihamu haki zao wanapokuwa safarini ambapo amezitaja baadhi ya haki hizo ni pamoja na abiria anapaswa  kupanda gari lililokuwa salama,kuepuka kupanda gari lililokuwa limejaa, kutokubuguziwa na watoa huduma pamoja na kutokupitilizwa kituo anachoshuka

Sauti ya Mwenyekiti wa Chama cha kutetea abiria nchini (TAKUHA)

Aidha Nkigi amewataka abiria kutokuwa waoga na kupaza sauti zao wanapoona kunachangamoto zimetokea katika vyombo vya usafiri kama dereva kukimbiza gari kwakutoa taarifa katika vyombo vya sheria ikiwemo jeshi la polisi kikosi cha usalama Barabarani pamoja na Chama cha kutetea abiria nchini  TAKUHA ili kupatiwa msaada.

Sauti ya Mwenyekiti wa Chama cha kutetea abiria nchini (TAKUHA)