Manyara yatajwa kuwa chini ya mikoa yenye vyoo bora nchini
10 July 2024, 5:59 pm
Baada ya Serekali kuzindua kampeni ya awamu ya pili ya mtu ni afya may 5 2024 na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Philip Mpango wanachi mkoani Manyara wametakiwa kujenga vyoo bora na kunawa mikono kwa maji tiririka na sabauni ili kuondokana na magonjwa ya mlipuko.
Na Hawa Rashid
Asilimia 77.4 ya kaya nchini inavyoo bora na asilimia 22.6 haina vyoo bora ambapo wananchi mkoani Manyara wametakiwa kujenga na kutuma vyoo bora ili kuepuka magonjwa yanayo ambukiza na yasiyo ambukiza ikiwemo huhara damu pamoja na magonjwa ya mfumo wa hewa.
Hayo yamesemwa na Mratibu wa kampeni ya Taifa ya usafi wa mazingira na kampeni ya mtu ni Afya Anyitike Mwakitalima kutoka Wizara ya Afya alipokuwa akizungumza na fm Manyara, amesema kampeni ya awamu ya pili ya mtu ni afya imezinduliwa rasmi may 5 2024 na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Philip Mpango na kuna maeneo tisa katika kampeni hiyo.
Aidha,amesema katika mikoa 26 ya Tanzania mkoa unaoongoza kwakua na vyoo bora na iliyo katika tano bora ni mkoa wa Dar es salaam ambao una asilimia 99.8 ikifuatiwa na mkoa wa Iringa ambao una asilimia 95.9, mkoa wa Kilimanyaro asilimia 92.5 mkoa wa Songwe asilimia 87.6 pamoja na mkoa wa Njombe una asilimia 86.5 nakusema mikoa iliyo katika tano bora ya chini ni Arusha ambao una asilimia 66.4 na Manyara 65.6 kutokana na takwimu za Wizara ya Afya kwa mwaka 2024.
Kwa upande wake Afisa Afya mkoa wa manyara Suten Mwabulambo amesema mkoa wa Manyara umejipanga kutekeleza kampeni hiyo ya mtu ni afya nakuwataka wananchi ambao hawajajenga vyoo bora kubadilika ili kuepuka magonjwa nyemelezi pamoja na wananchi kutoa taarifa katika Mamlka husuka kutokana na wananchi ambao hawana vyoo.