Magereza Babati yatimiza agizo la Rais Dk Samia
9 July 2024, 4:34 pm
Na George Augustino
Baada ya agizo la Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassankuzitaka taasisi zote za serikali ikiwemo magereza kuacha kutumia kuni na mkaa na badala yake kutumia nishati safi ya kupikia ili kutunza mazingira Jeshi la magereza Babati latimiza agizo hilo.
Kamishna wa utawala na rasilimali watu Jeshi la Magereza CP Jeremiah Katungu amezindua mradi wa nishati mbadala ya kupikia ya gesi vunde (Biogas) katika gereza la wilaya ya Babati mkoani Manyara ili kuondokana na matumizi ya kuni katika kupika chakula cha wafu gwa Magerezani na kuanza kutumia nishati safi ya gesi vunde.
Akizungumza na fm Manyara baada ya kukagua na kuzindua mradi huo CPKatungu amesema hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassankwa taasisi zote za serikali ikiwemo magereza kuacha kutumia kuni na mkaa ili kuendelea kutunza mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi kwa kutumia nishati safi.
Aidha CP katungu amesema matumizi ya nishati safi ya kupikia yatapunguza uharibifu wa mazingira na ukati wa miti hovyo kutokana kwa sasa upatikanaji wa kuni umekuwa na gharama.