FM Manyara

 Serikali yatoa bil.4 ujenzi shule ya wavulana Manyara

28 June 2024, 6:50 pm

Picha ya Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga akizundua shule ya sekondari ya wasichana Manyara

Sendiga azindua shule ya sekondari ya wasichana ya mkoa wa Manyara ambayo inatarajia kupokea wanafunzi wakike 142 wa kidato cha tano wa mchepuo wa masomo ya Sayansi kutoka mikoa mbalimbali nchini.

Na George Augustino

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga amesema Rais wa jamhuri wa muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa kiasi cha Shillingi Billioni 4 kwaajili ya ujenzi wa shule ya wavulana ya mkoa wa Manyara baada ya kuridhishwa na  ujenzi wa shule ya wasichana ya mkoa wa Manyara iliyojengwa katika Halmashauri ya mji wa Babati  mkoani Manyara iliyogharimu Shilingi Billioni 3.

Sendiga ameyasema hayo leo june 28 2024 alipokuwa akizindua Shule ya Sekondari ya wasichana ya mkoa wa Manyara ambayo inatarajia kupokea wanafunzi wakike 142 wa kidato cha tano wa mchepuo wa masomo ya Sayansi kutoka mikoa mbali mbali hapa nchini, amesema kutokana na juhudi walizo zionyesha katika usimamizi wa fedha, na ujenzi wa majengo ya shule hiyo yenye viwango Rais Samia ameamua kuwaongezea fedha nyingine kwaajili ya ujenzi wa shule ya wavulana .

Aidha mkuu wa Mkoa Manyara Sendiga amewaagiza wakuu wa Wilaya zote za mkoa wa manyara kwenda kusimamia utowaji wa huduma bora za elimu shule zinapofunguliwa katika ubora, maadili, taratibu, miongozo, sheria na kusimamia utoaji wa vyakula mashuleni pamoja na nayale shule zimekubaliana na kamati za shule.

Sauti ya Mkuu wa mkoa wa Manyara

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Babati Lazaro Jacobo Twange amezishukuru Taasisi mbalimbali za Serikali za mkoa wa Manyara ikiwemo Shirika la Umeme nchini Tanesco, Wakala wa Barabara nchini Tanroads na Mamlaka ya Maji safi na Uasafi wa Mazingira Bawasa kwa ushirikiano wao katika kutekeleza ujenzi wa Shule hiyo.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Babati