Wanahabari Manyara wanolewa mradi bomba la mafuta
19 June 2024, 6:51 pm
Ili kutekeleza mradi wa bomba la mafuta hoima Uganda hadi jiji Tanga na mkoa wa Manyara waandishi wa habari mkoani Manyara watakiwa kuendlea kutoa elimu kwa jamii kuhusu mradi huo na manufaa yake.
Na Geogre Augustino
Zaidi ya asilimia 99 ya wananchi wa mikoa ya Tanzania ikiwemo mkoa wa Manyara iliyopitiwa na mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi jijini Tanga nchini Tanzania wamepatiwa fidia ili kupisha mradi huo ambao unaendelea kufanyiwa kazi .
Afisa mawasiliano wa mradi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika mashariki (EACOP) Abass Abraham ameyasema hayo leo june 19 2024 alipokuwa akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari wa mkoa wa Manyara kuhusu utekelezaji wa mradi huo katika maeneo yaliyopitiwa na mradi na kuwataka kuwa mabalozi wa kutoa elimu kwa jamii kuhusu mradi huo unavyotekelezwa na manufaa yake.
Kwa upande wake mratibu wa ushirikishwaji jamii kwa mkoa wa Manyara wa mradi huo wa bomba la mafuta ghafi Emily Msisiri amesema mradi huo umepita katika kata mbili za wilaya ya Hanang’ zenye kilomita 17 na kilomita 106 katika maeneo ya kiteto pamoja na kilomita 6 katika wilaya ya Simanjiro ampapo kote wananchi wamelipwa fidia kwa kupewa fedha taslimu au kujengewa nyumba mbadala za kuishi zenye hadhi ya juu zaidi.