FM Manyara

Wananchi Manyara watakiwa kudumisha amani, kuliombea taifa

June 18, 2024, 6:47 pm

Picha ya Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alhaj Sheikh Muhamed khamis Kadidi

Wakati wa umini wa dini ya kiislam Mkoani Manyara wakisherekea sikukuu ya E al-adha Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Manyara amewataka kusheherekea sikukuu hiyo kwa kudumisha amani iliyopo nchini bila kuvunja sheria ya nchi na kuliombea taifa.

Na Hawa Rashid

Waumini wa dini ya kiisalam mkoani Manyara wametakiwa kusheherekea sikukuu ya  Eid  al-adha kwa amani na utulivu  bila kuvunja amani pamoja na kuliombea Taifa na kumuombea Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan aendelee kuliongoza Taifa kwa amani.

 Hayo yamesemwa Juni 17 2024 na Sheikh Mkuu wa mkoa wa Manyara Alkhaj Shekhe Muhamed Kadidi baada ya swala ya Eid al-adha iyoyoswaliwa katika uwanja wa Tanzanite kwaraa mkoani Manyara, amesema kwakua sikukuu hii ni sikuu ya kuchinja hivyo kwa muislam mwenye uwezo anaweza kuchinja mnyama kama Ngamia kondoo,Mbuzi au Ng’ombe ili kushikamana na sunna ya Baba wa iman nabii Ibrahim na mtume Muhamad ambapo mchinjaji atakula na familia yake pamoja na watu waaina mbali mbali.

Sauti ya Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Manyara

 Aidha Shekhe Kadidi ameawataka waumini wa dini ya kiislam mkoani Manyara kuendela kudumisha amani na kusheherekea sikuku ya Eid al-adha kwa furaha bila kumuudhi mwezi mungu kwa kuepuka  kufanya vitendo viovu pamoja na vitendo  vya uvunjifu wa amani.

Sauti ya Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Manyara