Wakulima mkoani Manyara watakiwa kuuza Mazao kwa kutumia Mizani
13 June 2024, 4:47 pm
Wakala wa vipimo mkoa wa Manyara unajukumu la kumlinda mlaji kwa kupima mizani zote za wafanyabiashara ili mkulima auze mazao yake na kupata fedha kulingana na thamani ya mazao yake aliyolima
Na George Augustino
Wakulima mkoani Manyara wametakiwa kuuza mazao mbali mbali kwa Wafanyabiashara kwakutumia mizani zilizohakikiwa na wakala wa vipimo mkoani hapa na kuachana na vipimo batili ili kuepuka kuibiwa na wafanyabiashara hao.
Meneja wa vipimo mkoa wa Manyara Denis Misango ameyasema hayo wakati akizungumza na Fm Manyara amesema jukumu lao kubwa ni kumlinda mlaji kwa kupima mizani zote za wafanyabiashara ili mkulima auze mazao yake na kupata fedha kulingana na thamani ya mazao aliyouza .
Aidha Misango amesema mazao yote yanayonunuliwa yanatakiwa kufungashwa kwa uzito unaokubalika kwa mujibu wa sheria ya vipimo ambapo mazao yote ya shambani yanatakiwa kufungashwa kwa uzito usiozidi kilo 100 na gunia likizidi kilo105 ni kosa kisheria na mfanyabiashara huyo anatakiwa kuchukuliwa hatua za kisheria