FM Manyara

Bodi ya Maji Bonde la Kati yaombwa  kuweka mipaka kwa Wananchi

June 11, 2024, 11:20 am

Picha ya Wadau wa Jumuiya za watumia Maji Kidaka ziwa Manyara

kutokuwepo kwa mipaka ya vyanzo vya maji kunapelekea wananchi kufanya shughuli za kibinaadamu kwenye vyanzo vya maji na kusababisha uharibifu wa kukauka kwa vyanzo hivyo.

Na Christina Christian

Wadau wa Jumuiya za watumia maji Kidaka ziwa Manyara wameiomba Bodi ya maji Bonde la kati kwa kushirikiana na serikali wawaainishie mipaka ya vyanzo vya maji ili kuendelea kutunza vyanzo hivyo.

Wakizungumza katika kikao cha uundaji wa kamati ya kidaka maji kilichofanyika katika ukumbi Goodlife wilayani Babati mkoani Manyara, wamesema kutokuwepo kwa mipaka hiyo kunapelekea watu kufanya shughuli za kibinaadamu kwenye vyanzo vya maji na kusababisha uharibifu wa kukauka kwa vyanzo hivyo.

Wamesema mipaka itakapoonyeshwa itasaidia  utendaji wa kazi kwakua mwananchi atakuwa na uelewa wa namna  ya utunzaji wa vyanzo vya maji nakufahamu umuhimu wa kuvilinda na kupunguza migogoro.

Sauti za wadau wa jumuia za watumiamaji

kwaupande wake Afisa maendeleo ya jamii Bodi ya maji Bonde la kati Nelea Bundala amesema wananchi wamekuwa wakichanganya mipaka ya vyanzo vya maji hali inayopelekea kipindi cha mvua nyingi maji yanaporudi katika maeneo yake ya asili wananchi  hulalamika  kwakusema wamevamiwa na maji.

sauti ya Afisa maendeleo ya jamii Bodi ya maji Bonde la kati

Aidha kikao cha uundaji wa kamati ya Kidaka maji kimehusisha wadau mbalimbali wa Jumuiya za watumia maji kikiongozwa na kaulimbiu isemayo” UTUNZAJI WA VYANZO VYA MAJI NI JUKUMU LETU SOTE”.