Wamiliki wa Vyombo vya moto mkoani Manyara watakiwa kuwa na Bima
7 June 2024, 2:11 pm
Jeshi la polisi kitengo cha usalama Barabarani Mkoani Manyara kimeendelea kutoa elimu kwa wamiliki wa magari kuwa na Bima za magari ili kuwasaidia wanapopata ajali na kutoa elimu kwa watembea kwa miguu
Na Hawa Rashid
Wamiliki wa vyombo vya moto mkoani manyara wametakiwa kuvikatia Bima vyombo vyao vya moto ili kumsaidia mmiliki wa chombo cha moto kifidiwa na bima hiyo pindi anapopata ajali ikiwemo kuharibika au kusababisa vifo.
Wito huo umetolewa na mkaguzi msaidizi wa polisi Henrica Bonifasi kutoka kikosi cha usalama barabarani mkoani Manyara, alipokuwa akizungumza na fm Manyara, amesema kuna aina mbili za Bima ikiwemo Bima ya lawama ambayo nilazima wamiliki wa vyombo vya moto kuwa nayo kwakua inamsaidia aliyepata ajali iliyohusishwa na dereva kumsaidia ,na bima nyinyine ni Bima kubwa inayomsaidia mmliki pindi chombo chake kinapopata ajali kurudishiwa chombo kipya.
kwa upande wake Koplo Kimbwengo Zacharia kutoka dawati la elimu wilaya ya Babati kitengo cha usalama Barabarani,amesema waathirika wakubwa wa ajali za Barabarani ni watembea kwa miguu na wanawajibu wa kuwapa elimu ya usalama Barabaranii ili kupunguza ajali za Barabarani.
Aidha amesema mtembea kwa miguu anapaswa kuwa na elimu ya kutosha na kuwa makini anapokuwa Barabani na sehemu sahihi anayotakiwa kuvuka amapokuwa Barabarani ni katika eneo la kivuko isipokuwa eneo la makutano ya Barabara yanapokuwa magari ambapo hapaswi kuvuka.