CCM Mkoani Manyara yasikia kilio cha wanachi wa maretadu na labay
30 May 2024, 6:43 am
Baada ya changamo ya muda mrefu ya kukosa daraja kwa wakazi wa vijiji viwili vya maretadu na labay wilayani Babati mkoani Manyara hatimaye changamoto hiyo imetatuliwa.
Na Emmy Petter
Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Manyara kwa kushirikiana na Serekali ya mkoa wamezindua daraja la kisasa katika bara bara ya garkawe katika kata ya maretadu lililokuwa na changamoto ya kuvuka kwa muda mrefu.
Akizungumza baada ya kukagua daraja hilo Meneja wa Tarula wilaya ya mbulu mhandisi Tono Hondo amesema lengo la kujenga daraja hilo la kisasa nikurudisha mawasiliano kati ya kata ya maretadu na labay kwa kuunganisha kata hiyo na makao makuuu ya Halmashauri ya dongobeshi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Manyara Peter Toima amesema wameridhishwaa na utekelezaji wa mradi huo wa daraja kwa kuzingatia ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM kinachoongozwa na Rais Dk Samia Suluhu Hassan.
Aidha, baadhi ya wananchi wakata hizo mbili wameishukuru serekali kwa kuwa tengenezea daraja hilo kwakua walikuwa wakipata adharaa ya kulala mbali ya nyumba zako kipindi cha mvua pamoja na kushindwa kupeleka mazao yao sokoni nyakati wa mavuno.