FM Manyara yagawa taulo za kike kwa wafungwa, wanafunzi
28 May 2024, 10:16 pm
Leo ikiwa ni Siku ya Hedhi Salama duniani mabinti na wanawake wote kwa ujumla wametakiwa kujihifadhi kwakutumia taulo za kike, FM Manyara radio imetembelea na kugawa taulo za kike kwa wanafunzi pamoja na wafungwa wanawake wilayani Babati mkoani Manyara na kuwaasa kuwa wasafi muda wote.
Na Hawa Rashid
Ikiwa Dunia inaadhimisha siku ya hedhi salama wafanyakazi wa wa Fm Manyara radio wilayani Babati mkoani Manyara leo wametembelea shule ya sekondari Magugu iliyopo Halmashauri ya wilaya ya Babati mkoani hapa pamoja na gereza la mkoa wa Manyara kugawa taulo za kike kwa wanafunzi pamoja na wafungwa wa kike.
Akizungumza baada ya zoezi la kugawa taulo hizo Mkurugenzi mtendaji wa Fm Manyara radio Esther Mgonja amesema fm manyara imeguswa kwa kutoa taulo hizo kwa mabinti na wafungwa wanawake ili wajisitiri wanapokuwa katika siku zao za hedhi
Aidha ameishukuru ofisi ya mkuu wa mkoa wa Manyara kwa ushirikiano ili kufanikisha zoezi hilo.
Kwa upande wake Mwalimu wa shule ya Magugu Sekondari Devota Msigwaameishukuru Fm Manyara radio kwa kuwapelekea taulo hizo za kike mabinti shuleni hapo nakusema zitawasaidia mabinti hao wanapokuwa katika siku zao kwakua wengi hushindwa kwenda shule wanapokuwa katika hali hiyo kwa kushindwa kujihifadhi vizuri.
Aidha baadhi ya wanafunzi wa kike wa shule hiyo wameishukuru Fm manyara kwa kuona umuhimu wa kuwapa taulo za kujihifadhi wanapokuwa katika siku zao za hedhi na kuwashauri mabinti kuwa wasafi wakati wowote.