FM Manyara

Jamii  yatakiwa kuondoa tofauti zao kumlinda mtoto

10 May 2024, 8:39 pm

Picha ya Afisa maendeleo ya jamii Halmashauri ya mji wa Babati

Kuongezeka kwa vitendo vya kikatili  na mmommonyoko wa maadili vinasababishwa na baadhi ya wazazi wanapogombana ambapo familia nyingi huathirika kwa kukosa malezi bora na  muelekeo mzuri katika maisha yao

Na Marino Kawishe

Kuelekea siku ya familia duniani  ambayo huadhimishwa kila ifikapo may 15, wazazi na walezi wilayani Babati wametakiwa kumaliza tofauti zao ili kutoathiri  malezi na makuzi ya watoto na kumlinda mtoto dhidi ya ukatili, pamoja na kumpatia mahitaji ya msingi.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa maendeleo ya jamii Halmashauri ya mji wa Babati Diana Mchonga alipokuwa akizungumza na fm Manyara katika kipindi cha Mseto wa Leo,amesema inapotokea wazazi wanagombana hali hiyo inawathiri kwa kiasi kikubwa watoto na kukosa muelekeo sahihi katika maisha yao.

Sauti ya Afisa maendeleo ya jamii Halmashauri ya mji wa Babati

Kwa upande wake Afisa ustawi wa Jamii Halmashauri ya Babati mji Damian Nyamako  amesema kuelekea kilele cha siku ya Familia watatumia  vyombo vya habari kuelimisha jamii kuhusu maswala mbali mbali ya ukatili kwa jamii, sheria na haki za wototo pamoja na malezi bora katika familia zao.

Sauti ya Afisa ustawi wa Jamii Halmashauri ya Babati mji

Nae Mwenyekiti wa SMAUJATA (Shujaa wa maendeleo na ustawi wa jamii Tanzania)  mkoa wa Manyara Philipo Sanka amesema wazazi wawalee watoto wao wenyewe na sio kuwapeleka kwa bibi zao kwenda kulelewa  na wataendelea kuchukua hatua stahiki wahusika wanaofanya vitendo vya kikatili kwa watoto na kuwaripoti katika vyombo vya kisheria.

Sauti ya Mwenyekiti wa SMAUJATA mkoa wa Manyara

Aidha kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya familia duniani inasema “Tukubali tofauti zetu kwenye familia;Kuimarisha malezi ya watoto”