CCM yashindwa kusimamia miundombinu ya stendi ya Noah Babati mji
3 May 2024, 6:45 am
Licha ya juhudi za wafanyabiashara mbali mbali wakiwemo mama lishe wanaofanya biashara zao katika stendi ya Noah iliyopo Babati mji kuomba uwongozi wa Chama cha Mapinduzi Ccm Babati mji kuboresha mazingira ya eneo hilo linalotuama maji machafu nakuhatarisha afya zao lakini juhudi zao zimegonga mwamba.
Na Marino Kawishe
Wananchi wanaofanya biashara katika eneo la stend ya Noah lililopo katika kata ya Bagara Halmashauri ya mji wa Babati wameiomba serikal ya Chama cha Mapinduzi Ccm kuboresha miuondo mbinu ya eneo hilo linalotuama maji machafu yanayotishia afya zao pamoja na kuomba kujengewa choo kwenye eneo hilo
Wakizungumza na Fm Manyara wafanyabiashara hao wamesema wanafanya biashara zao kwa tabu katika eneo hilo kutokana na maji kutuama hali inayopelekea kutoa harufu kali inayoambatana na mazingira machafu licha yalikupa kodi pamoja na ushuru kwa wasimamizi wa eneo hilo lakini mpaka sasa hakuna juhudi zozote zilizo chukuliwa katika eneo hilo,.
Kwa upende wake katibu wa Chama cha Mapinduzi Ccm Babati mji Mohamed Chollaje alipotafutwa na mwandishi wa habari hii ili kuzungumzia swala hilo alishindwa kutoa ushirikiano na badala yake alisema yupo kwenye kikao licha kutafutwa kwa mara nyingine.
Aidha, Afisa afya wa Halmashauri ya Mji wa Babati Emmanuel Kimonge amesema eneo hilo lipo chini ya Chama cha Mapinduzi Ccm ambapo wameshawaandikia barua kwaajili ya kuweka vifusi katika eneo hilo ili kuweka mazingira salama na wamewaelekeza mama lishe kufuata taratibu za kiafya kwa kuwa na vyakula vya moto pamoja na maji ya moto ili kuwa salama.