Zimamoto yatoa tahadhari ya mvua Manyara
18 April 2024, 12:05 pm
kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kuleta madhara katika maeneo mengi nchini wananchi wanaoishi mabondeni wametakiwa kuhama
Na Emmy peter
Wananchi mkoani Manyara wametakiwa kuendelea kuchukua Tahadhari kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini kwa baadhi ya maeneo ambapo barabara na madaraja yanajaa maji katika maeneo wanayoshi.
wito huo umetolewa leo na Kamanda wa jeshi la zima moto na uwokoaji mkoa wa Manyara Kamishna msaidizi Gilbert Mvungi alipokuwa akiongea na fm Manyara, amesema kwa wananchi wa mkoa wa Manyara waliopo mabondeni mvua zinaponyesha maji yanajikusanya katika maeneo yao ambapo wanapaswa kuchukua tahadhari ikiwemo kuondoka maeneo waliopo au walipojenga.
Kamanda Mvungi amesema wazazi wanapaswa kuwaangalia watoto wao wanapopita katika madaraja kwakua kunamadaraja rasmi na madaraja ya siyo rasmi yaliyowekwa magogo na katika kipindi hiki chamvua kumekuwa na changamoto nyingi za madaraja kujaa maji.
Aidha, amesema jeshi la Zimamoto na uwokoajia mkoa wa Manyara linaendelea kutoa elimu katika vyombo mbali mbali vya habari ikiwemo katika radio,runinga magazeti na mitandao ya kijamii.