Mitandao ya kijamii yachangia mmomonyoko wa maadili
18 April 2024, 11:44 am
Sababu ya kuongezeka kwa mmomonyoko wa maadili kwa watoto yatajwa wazazi ndio sababu kubwa kwa kuwaachia simu za mkononi watoto wao.
Na George Augustino
Jamii mkoani Manyara imetakiwa kuwalea watoto wao katika misingi imara na yenye maadili ya kitanzania kwa kuwaepusha kutumia simu za mkononi ili kujenga kizazi chenye maadili mema na kuepuka kesi za mitandao ya kijamii.
Hayo yamesemwa leo na Meneja wa Mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA kanda ya kaskazini Mhandisi Fancisi Mihayo alipokuwa akiongea katika kipindi cha Mseto wa leo kinachorushwa na Fm Manyara Radio, amesema asilimia kubwa kwa sasa watoto wanalelewa na simu za mkononi ambapo wazazi huwapa watoto wao uhuru wakutumia simu nakuingia katika kurasa za mitandao ya kijamii hali ambayo si nzuri kwa malezi ya mtoto.
Aidha, Injia Mihayo amewataka wazazi kuwa makini katika malezi ya watoto wao kwa kudhibiti matumizi ya simu na kuacha kuweka picha ambazo hazina maadili katika mitandao yao ya kijamii.