Mshauri (TCCIA ) Manyara kizimbani
24 March 2024, 1:34 pm
Mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Manyara ya muachia huru Mshauri wa Wafanyabiashara TCCIA
Na Mzidzlifa zaid
Mahakama ya Hakimu Mkazi Manyara imemhukumu Ramadhani Rashid Msangi Mshauri wa Wafanyabiashara wa Chama cha wenye viwanda na kilimo Mkoa wa Manyara (Bussines consultant -TCCIA Manyara) kwenda jela miaka mitatu au kulipa kiasi cha shilingi 900,000 kwa kosa la kughushi nyaraka za malipo .
Hukumu hiyo dhidi ya Ramadhani Rashid Msangi katika shauri la uhujumu uchumi na. 05/2023, imetolewa na hakimu Mkazi wa Mahakama ya Manyara Martin Massao Machi 22, 2024.
Hakimu Massao amesema Mshtakiwa huyo alighushi nyaraka mbali mbali katika marejesho yake kuonyesha kuwa alihudhuria na kuendesha mafunzo ya wajasiriamali yaliyofanyika wilayani Hana’ng mkoani Manyara kwa kipindi cha mwezi februari na juni mwaka 2018 ambapo alitumia kiasi cha shilingi 6,695,000 Kugharamia posho ya chakula , ukumbi na nauli kwa waliodaiwa kushiriki mafunzo hayo na akijua taarifa hizo hazikuwa sahihi.
Aidha,mshitakiwa amelipa faini na kuachiwa huru na mahakama hiyo.