Wananchi acheni kuwaficha wahalifu
20 March 2024, 5:27 pm
Polisi Manyara yawataka wananchi kuripoti matukio ya kihalifu katika mitaa yao.
Na George Agustine
Wananchi wilayani Babati mkoani Manyara wametakiwa kutoa taarifa katika kituo cha polisi kutokana na watu wanaofanya matukio ya kihalifu katika mitaa yao ili wachukuliwe hatua za kisheria na kukomesha matukio hayo.
Akizungumza na Fm Manyara katika kipindi cha Mseto wa Leo mkuu wa kituo cha polisi wilaya ya Babati Amiri Mlemba,amesema wananchi wanapaswa kuwaripoti wahalifu waliopo majumbani badala ya kuwahifadhi na kuacha vitendo hivyo kuendelea ambapo amesema jeshi la ulinzi shirikishi kwa kusaidiana na jeshi la polisi wamefanikiwa kuwakamata wahalifu nyakati za usiku.
Aidha Mlemba amewataka waendesha pikipiki maarufu bodaboda kuwa waangalifu hasa nyakati za usiku kwa kutoa taarifa katika kituo cha polisi kabla hawajaanza safari yakuwapeleka abiria.
kwa upande wake mratibu wa dawati la jinsia wilaya ya Babati Koplo Leokadia Mmanya, amesema ili kudhibiti vitendo vya uharifu mzazi anapaswa kumlea mtoto kwa maadili ili anapokua asijiingize kwenye makundi ya kiuharifu.
.