FM Manyara

Kichanga chaokotwa katika shimo la kuhifadhia maji taka Babati

February 23, 2024, 5:41 am

Mwili wa mtoto mchanga umeokotwa leo katika chemba ya kuhifadhia maji taka mkoani Manyara

Na Emmy perter

Mwili wa mtoto mchanga umeokotwa leo katika chemba ya kuhifadhia maji taka katika mtaa wa mji mpya nyumba ya ndugu Raeli wanayoishi wapangaji  katika kata ya Maisaka wilayani Babati mkoani Manyara.

Mwenyekiti wa mtaa  huo John Mosko  amesema alipata tarifa hizo  kutoka kwa mjumbe wa serikali za mitaa kuwa kuna kiumbe ambacho kimekutwa katika shimo la maji taka  ambacho kina sadikika kuwa na miezi miwili hadi mitatu.

Aidha,mwenyekiti  huyo ,amesema hilo ni tukio latatu kutokea katika mtaa wake na baada ya kutokea  walitoa taarifa polisi ambapo walikuja kuuchukua mwili huo na aliyefanya tukio hilo bado hajabainika.

Sauti ya mwenyekiti

Nao baadhi ya majirani akiwemo mjumbe wa mtaa huo, wamesema kitendo hicho ni kibaya ambapo wameliomba jeshi la polisi kuwachukulia hatua za kisheria waliohusika na tukio hilo.

Sauti ya majirani