FM Manyara

Polisi Manyara watumia mabomu ya machozi kutawanya wananchi

February 21, 2024, 5:57 pm

Wananchi wa kata ya Magugu walivyoondamana kupinga vitendo vya mauaji

Jeshi la polisi mkoani Manyara lalazimika kutumia mabomu ya machozi  kuwatawanya wananchi walioandamana bara bara kuu ya Babati -Arusha kufuatia kuuliwa kwa mtoto wa miaka saba

Jeshi la polisi mkoani Manyara limelazimika kutumia mabomu ya machozi  ili kuwatawanya wananchi waliokuwa wameandamana katika bara bara kuu ya Babati –Arusha wakizuia magari ya abiria kupita kufuatia kuuliwa kwa mtoto wa miaka saba

Wananchi  hao wa kata ya Magugu wilayani Babati mkoani Manyara, wamesema  wamelazimika kuandamana hadi katika kituo cha polisi cha Magugu wakipinga jeshi la polisi mkoani hapa kumpeleka mtuhumiwa kituo cha polisi nakutaka kumuua kwakua watuhumiwa wengi  wanaachiwa  huru.

Sauti ya wananchi wa kata ya Magugu

Aidha  kufuatia ghasia hizo kamanda wa jeshi la polisi mkoani Manyara George Katabazi amelazimika kuongeza nguvu ya maaskari ili kutuliza wananchi na kupata suluhu ya kuzungumza nao kwa njia ya amani huku akielezea kilichojiri katika eneo la tukio.

Sauti ya kamanda wa jeshi la polisi mkoani Manyara

Mapema asubuhi kamanda Katabazi  alifika katika kijiji hicho kutoa pole kwa wanafamilia, na kuahidi  jeshi la polisi halitamfumbia macho mtuhumiwa yeyote atakaehusika na vitendo vya kiharifu katika kata hiyo ya  Magugu na kutoa gari katika kituo cha polisi Magugu ili lisaidia kuimarisha hali ya ulinzi na usalama.