Tosci yawataka wakulima kutoa taarifa wanapouziwa mbegu zisizo na ubora
16 February 2024, 7:21 pm
Wananchi mkoani Manyara wametakiwa kutoa taarifa kwa Taasisi ya kudhibiti ubora wa mbegu Tanzania (TOSCI) wanapobaini wameuziwa mbegu bandia.
Na Mzidalfa Zaid
Wananchi mkoani Manyara wametakiwa kutoa taarifa kwa Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) wanapobaini wameuziwa mbegu bandia au ambazo hazina ubora.
Wito huo umetolewa leo na mmkaguzi wa mbegu kutoka (TOSC)I kanda ya kaskazini Nicodemas Tlankka wakati akiongea na waandishi wa habari mkoani Manyara katika kikao cha utoaji wa elimu kuhusu ubora wa mbegu.
Amesema mkulima anapofika katika duka la uuzaji wa mbegu ili kutambua mbegu kama ni feki mfuko huo unakuwa hauna lebo ya (TOSCI) au OECD,hakuna taarifa muhimu kama jina, aina ya zao, daraja la mbegu, jina la mzalishaji, tarehe ya majaribio, au mfuko kufunguliwa.
Kwa upande wake mkaguzi kutoka (TOSCI) makao makuu morogoro Frank Maxmilian amesema lengo la kuwakutanisha waandishi wa habari ni ili kuwapa elimu ambayo wataifikisha kwenye jamii .