FM Manyara

Siku ya mbolea duniani kuadhimishwa kitaifa Manyara

27 September 2024, 6:39 pm

Mamlaka ya udhibiti wa mbolea Tanzania (TFRA) imewataka wananchi mkoani Manyara kushiriki maonesho ya siku ya mbolea duniani ili wajionee fursa mbalimbali zitakazokuwepo.

Na Mzidalfa Zaid

Kuelekea Siku ya Mbolea Duniani ambayo inatarajiwa kuadhimishwa kitaifa mkoani Manyara , wadau mbalimbali wametakiwa kushiriki maeonesho hayo, ambayo yanatarajia kuanza Oktoba 10 hadi 13  mwaka huu na  mgeni rasmi wa kilele cha maonesho hayo anatarajiwa kuwa Waziri wa Kilimo Hussen Bashe.

Akiongelea maandalizi ya maoenesho hayo Meneja Uhusiano, Mawasiliano na Elimu kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Matilda Kasanga, amesema maoenesho ya mwaka huu yamekuwa tofauti kwa kuwa kutakuwepo kongamano la kwanza la mbolea Oktoba 11 hadi 12 mwaka huu ambapo kutakuwepo wataalam mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi .

Sauti ya Meneja Uhusiano, Mawasiliano na Elimu FRA Matilda Kasanga

Kwa upande wake Meneja wa TFRA Kanda ya Kaskazini Gothard Liampawe, amewataka wadau mbalimbali wa kilimo kushiriki maoneosho hayo kwakuwa kutakuwepo watalaam ambao watatoa elimu inayohusu matumizi sahihi ya mbolea.

Sauti ya Meneja wa TFRA Kanda ya Kaskazini Gothard Liampawe

Aidha, mwakilishi wa ruzuku wa TFRA mkoa wa Manyara Muhamed Bakari Saidi amesema kama kuna mwananchi anahitaji kuwa wakala wa kusambaza mbolea afike kwenye ofisi za TFRA mkoa wa Manyara ili apate mafunzo na biashara yake kusajiliwa ili apate kibali cha kuuza mbolea. 

Sauti ya mwakilishi wa ruzuku wa TFRA mkoa wa Manyara Muhamed Bakari Saidi