FM Manyara

Maadhimisho ya damu salama kitaifa kufanyika Manyara

13 June 2024, 5:07 pm

Zoezi  la uchangiaji  limeanza  juni 1 2024 kwakuweka kambi katika maeneo mbali mbali ya mkoa wa Manyara na wananchi kuchangia damu pamoja na utoaji wa elimu ambapo kilele chake kitafanyika june 14 katika ukumbi wa CCM mkoa mkoani Manyara

Na Emmy Peter

Mkuu wa  mkoa wa Manyara  Queen Sendiga  amewataka wananchi mkoani Manyara kuchangia damu salama  kwakua zoezi hilo ni la hiyari na damu hiyo itawasaidia wenye uhitaji wakiwemo kinamama wajawazito, watoto pamoja na wanaopata ajali

Sendiga ameyasema hayo leo ofisini kwakwealipokuwa akizungumza na wandishi wa habarim kuelekea  siku ya  uchangiaji damu  salama  june 14 ambayo kitaifa  inafanyika  mkoani Manyara, amesema  mkoa wa Manyara ni miongoni mwa mikoa iliyo pewa kipaombele katika kuadhimisha siku hiyo na lengo la siku hiyo ni kuendelea kutoa elimu na kuhamasisha  jamii  kuchangi aji damu salama.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara

Sendiga  amesema zoezi hilo limeanza kuanzia juni 1 2024 kwakuweka kambi katika maeneo mbali mbali ya mkoa wa Manyara kwa wananchi kuchangia damu pamoja na utoaji wa elimu ambapo kilele chake kitafanyika june 14 katika ukumbi wa CCM mkoa mkoani Manyara ambapo wataalamu watakuwepo sehemu mbali mbali za vituo vya uchangiaji damu.  

Kwaupande wake Mganga mkuu wa mkoa Dokta Damasi Kayera  amesema zoezi la ukusanyaji wa damu katika mkoa wa Manyara unaendelea kuboreshwa  vizuri ambapo kwa mwaka jana mkoa wa Manyara ulikusanya asilimia 75 za damu salama nakusema wananchi wanatakiwa kuchangia  zaidi ya chuma 15,000 kwa mwaka.

Sauti ya Mganga Mkuu wa Mkoa

Nae mkuu wa idara ya damu salama  viwango na ubora kitaifa Dustan Haule amesema mtu anaestahili kuchangia damu awe na uzito wakuanzia kilo 50  kuendelea naasiwe na  magonjwa ya kudumu kama Presha, Kisukari na Saratani

Sauti ya Mkuu wa idara ya Damu Salama

Aidha,Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya damu salama duniani  kwa mwaka huu inasema ”MIAKA 20 YA UCHANGIAJI DAMU ASANTE KWA KUCHANGIA DAMU