Askari kata afariki kwa ajali Babati
24 December 2024, 5:07 pm
Askari kata wa kituo cha polisi Kiteto Geogre Mwakambonjo anaekediriwa kuwa na umri wa miaka 40 amefariki baada ya kugongwa na lori
Na Mzidalfa Zaid
Askari kata wa kituo cha polisi Kiteto Geogre Mwakambonjo anaekediriwa kuwa na umri wa miaka 40 amefariki baada ya kugongwa na lori akiwa kwenye pikipiki mchana wa leo katika eneo la Msasani Maisaka wilayani Babati mkoani Manyara barabara ya Arusha dodoma.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoani Manyara Ahmed Makarani amesema ajali hiyo imetokea baada lori iliyokuwa nyuma ya pikipiki hiyo kumgonga mwendesha pikipiki kwa nyuma na kusababisha kifo cha askari huyo aliyekuwa amebebwa na pikipiki hiyo ambapo amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa lori.
Shuhuda wa tukio hilo amesema ajali hiyo imetokea baada lori iliyokuwa nyuma ya pikipiki hiyo kumpigia honi hali iliyosababisha kupoteza uelekeo na kumgonga kwa nyuma na kusababisha kifo cha askari huyo.
Aidha, kamanda wa jeshi mkoani Manyara amesema hali ya ulinzi na usalama katika mkoa wa Manyara imeimarishwa na kuwataka wananchi kusherehekea sikukuu kwa amani na utulivu.