FM Manyara
FM Manyara
24 February 2026, 6:16 pm

Mfuko wa Maendeleo ya jamii PSSSF umeendelea kuboresha huduma zao kwa njia ya kidigital kwa kuwafikia maafisa utumishi na wahasibu katika mikoa kumi kwa kufikisha elimu kwa wanachama wa mfuko huo.
Na Emmy Peter
Hayo yamesemwa na Meneja wa PSSSF kanda ya kaskazini Yessaya Mwakifulefule alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ndogo za hazina zilizoko Mkoani Manyara, amesema mfuko wa PSSF umeendelea kuwaelimisha wafanyakazi kujiunga na mfuko huo ili kunufaika kipindi cha uzee.

Kwa upande wake Katibu tawala wa Mkoa wa Manyara Maryamu Muhaji amesema mafunzo hayo yatawasaidia waajiri pamoja na maafisa utumishi kuwaandaa watumishi wanaokaribia kustaafu ili kutatua matatizo ya ucheleweshaji wa mafao.
Aidha baadhi ya maafisa rasilimali watu wameushukuru mfuko PSSSF kwa kuwakutanisha katika mafunzo hayo na kuwapa elimu kuhusu mfuko na mafao yatokanayo na mwanachama ambapo wamesema watahakikisha michango ya mwanachama inakusanywa na kufikisha kwa wakati katika mfuko huo tofauti na ilivyokuwa awali.