FM Manyara

Mfumo wa e-mrejesho unavyohudumia wananchi kwa wakati

18 February 2026, 6:52 pm

Picha ya Naibu waziri, ofisi ya rais – menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora, mhe. Regina Qwaray na mkuu wa wilaya ya Babati Emmanuela Kaganda

Naibu waziri, ofisi ya rais – menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora, mhe. Regina Qwaray amesema serikali imeanzisha mfumo wa e-mrejesho ambao ni jumuishi unaomwezesha mwananchi kutuma,kufuatilia na kupokea mrejesho wa malalamiko,mapendekezo, maulizo au pongezi.

Na Mzidalfa Zaid

Amesema hayo leo katika kikao cha baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Babati, amesema mfumo huo utasaidia wananchi kutatuliwa changamoto zao kwa wakati.

sauti ya Naibu waziri, ofisi ya rais – menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora, mhe. Regina Qwaray

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Babati Emmanuela Kaganda , amesema changamoto zote ambazo zimeelezwa na madiwani zinafanyiwa kazi na kata zote zitafikiwa.

sauti ya mkuu wa wilaya ya Babati Emmanuela Kaganda

Aidha mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Babati John Noya, amewataka madiwani kusimamia miradi ya serikali kufuatia kuwepo kwa uharibifu wa miundombinu unaosababishwa na baadhi ya wananchi.

sauti ya mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Babati John Noya
0-4064×3074-0-0#