FM Manyara

Makosa 76 yaripotiwa Manyara ndani ya miezi 3

17/02/2026, 18:08

Picha ya kamanda wa jeshi la polisi  mkoa wa manyara Ahmed Makarani

Jumla ya makosa 76  yakiwemo  makosa ya mauaji, kubaka na ulawiti  yameripotiwa kutokea  mkoani  Manyara katika kipindi cha miezi mitatu  kuanzia mwezi wa kumi na moja mwaka jana 2025  hadi mwezi wa pili  mwaka huu 2026.

Na George Agustino

Taarifa hiyo imetolewa na kamanda wa jeshi la polisi  mkoa wa manyara Ahmed Makarani alipokuwa akizungumza katika kipindi cha mseto wa leo kinachorushwa na FM Manyara. Amesema  kwa ujumla hali ya usalama ni shwari ndani ya mkoa wa Manyara ambapo ndani ya kipindi hicho  makosa 15 ya mauaji, makosa 47 ya kubaka  na makosa 14 ya ulawiti ndiyo yaliyoleta  mshtuko  mkubwa  katika jamii.

Sauti ya kamanda wa jeshi la polisi  mkoa wa manyara Ahmed Makarani

Aidha kamanda Makarani amesema jeshi la polisi kupitia polisi jamii wamekuwa wakishirikiana  na jamii moja kwa moja katika kutoa elimu na kupokea taarifa mbalimbali kutoka kwa wananchi zikiwemo taarifa za matukio ya kiuhalifu  na kuzifanyia  kazi.