FM Manyara

Serikali yaendelea kutambua mchango wa vyombo vya habari

13 February 2026, 8:16 pm

Picha ya mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga

Leo ikiwa ni siku ya redio duniani, mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga amesema serikali inaendelea kutambua mchango wa vyombo vya habari kwa kuwa vinaelimisha jamii.

Na Mzidalfa Zaid

Akiongea na fm Manyara radio, Sendiga amesema mchango wa vyombo vya Habari zikiwemo redio zimekuwa na mchango mkubwa ambapo ameipongeza manyara redio kuelezea kazi kubwa zinazofanywa na serikali ambapo ameuomba uongozi wa fm Manyara radio kuendelea kufikisha elimu katika jamii.

sauti ya mkuu wa mkoa wa manyara queen Sendiga

Aidha, baadhi ya wadau mbalimbali wamesema fm Manyara ni chombo muhimu katika mkoa wa Manyara na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa redio hii.