FM Manyara

TMA Manyara yatoa mwelekeo wa mvua mwezi march –may

12 February 2026, 4:59 pm

PIcha ya mvua

Mamlaka ya hali ya hewa mkoa wa Manyara imesema kwa kipindi cha kuanzia mwezi march hadi mwezi mei kunatarajiwa kuwa na mvua za kiwango cha kawaida hadi wastani.

Na Mzidalfa Zaid

Akiongea na fm Manyara meneja wa TMA mkoa wa Manyara Salma Amour amesema kwa mkoa wa Manyara mvua inatarajia kuanza wiki ya pili ya mwezi march hadi mwezi mei na kiwango kikubwa cha mvua kinatarajiwa mwezi april.

Sauti ya meneja wa TMA mkoa wa Manyara Salma Amour
picha ya meneja wa TMA mkoa wa Manyara Salma Amour

Kwa upande wake mtabiri wa hali ya hewa mkoa wa manyara Haji Amimu, amewataka wananchi mkoa wa Manyara wakiwemo wakulima , wafugaji na wavuvi kuzingatia utabiri wa hali ya hewa unaotolewa na TMA ili uwasaidie katika shughuli zao za kila siku.

Sauti ya mtabiri wa hali ya hewa mkoa wa manyara Haji Amimu
picha ya mtabiri wa hali ya hewa mkoa wa manyara Haji Amimu