FM Manyara
FM Manyara
29 January 2026, 5:03 pm

Maafisa usafirishaji maarufu bodaboda pamoja na madereva wengine wa vyombo vya moto wilayani Babati mkoani Manyara wametakiwa kuzingatia sheria za usalama barabarani ili watumiaji wengine wa barabara waendelee kubaki salama.
Na Mzidalfa Zaid
Wito huo umetolewa na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Mrakibu wa Polisi Emmanuel Kandolla amesema oparesheni mbali mbali zinaendelea kufanyika kuhakikisha watumiaji wa barabara wanakuwa salama na wanaovunja sheria wanachukuliwa hatua za kuandikiwa tozo au kufikishwa mahakamani .
Aidha,Kandolla amesema bado wanaendelea kufanya oparesheni za kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria wahalifu ambao wanatumia nafasi za maafisa wasafirishaji nyakati za usiku kupora na kuwaibia watu pamoja na kutenda makosa ya jinai.