FM Manyara

Babati watakiwa kutoa taarifa wanapovamiwa na wanyamapori

22 January 2026, 7:04 pm

Picha ya afisa wanyamapori halmashauri ya wilaya ya Babati Samwel Bayo

Kufuatia kuwepo kwa changamoto ya wanyama kuvamia makazi ya watu na kuharibu mazao pamoja na kujeruhi binadamu katika halmashauri ya ya wilaya ya Babati, wito umetolewa kwa wanchi kutoa taarifa kunapotokea changamoto hiyo ili mamlaka husika ichukue hatua za haraka.

Na Mzidalfa Zaid

Wito huo umetolewa leo na afisa wanyamapori halmashauri ya wilaya ya Babati Samwel Bayo, wakati akiongea na FM Manyara, amesema mwananchi yeyote anapokumbwa na tatizo la kuvamia na wanyamapori afike kwenye ofisi za mwenyekiti wa kijiji ili uongozi wa kijiji utoe taarifa kwa Mamlaka husika ambayo itafanya tathimini kwa ajili ya kifuta jasho.

sauti ya afisa wanyamapori halmashauri ya wilaya ya Babati Samwel Bayo

Aidha, amesema madhara yatokanayo na wanyamapori yapo ambayo yamekuwa yakisababishwa na tembo, pundamilia na fisi likwemo tukio ambalo limetokea hivi karibuni la mtu mmoja kuuliwa na fisi.