FM Manyara
FM Manyara
21 January 2026, 5:29 pm

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga amezindua namba ya bure ya huduma kwa mteja ambayo itatumika kupokelea changamoto na kero au malalamiko ya wananchi wote wa mkoa wa Manyara.
Na Mzidalfa Zaid
Sendiga amezindua namba hiyo ambayo ni 0800787722 na kusema itasaidia kurahisisha kupokea changamoto nyingi kwa wakati na kuzifanyia kazi ambapo mwananchi atapiga namba hiyo bure bila malipo au makato yeyote na kutoa taarifa iliyosahihi pasipo kudanganya.
Aidha Sendiga amezitaka ofisi zote zilizopo chini yake kufanyia kazi kwa haraka na kuzipatia ufumbuzi changamoto zote watakazopokea na kurudisha taarifa katika ofisi ya mkuu wa mkoa ili kutunza ripoti na taarifa za kila mwezi.
