FM Manyara
FM Manyara
14 January 2026, 11:37 pm

Wakati shule zikiwa zimefunguliwa wiki hii wito umetolewa kwa wanafunzi kuchukua tahadhari za usalama barabarani kwa kuvuka na kutembea sehemu sahihi za kuvukia au kutembealea ili kuepukana na ajali.
Wito huo umetolewa na Afisa wa jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani kitengo cha utoaji elimu Sajenti Doto Aloyce, alipozungumza na Fm manyara amesema sehemu sahihi kwa wanafunzi kuvukia barabara ni kwenye alamaza pundamilia au aliposimama askari Polisi ambapo anaweza kusimamisha magari na wanafunzi wakapita kwa usalama.
Aiidha amewataka madereva Bodoboda kuacha kubeba wanafunzi wengi kwa wakati mmoja pindi wanapo wapeleka shule au kuwarudisha nyumbani sababu ubebaji huo sio rafiki kwa usalama wao, pia amewataka madereva hao kutowaachia au kuwapa wanafunzi waendeshe pikipiki wakati wa kwenda shule.
