FM Manyara

Zimamoto Manyara wapokea vitendea kazi

8 January 2026, 6:02 pm

Baadhi ya vifaa ambavyo vimepokelewa na jeshi la zima moto

Jeshi la zima moto na uokoaji mkoa wa Manyara limekabidhiwa vifaa vya kutendea kazi kwa ajili ya maokozi kunapotokea majanga mbalimbali ili jeshi hilo lifanye kazi kwa ufasaha na kwa wakati.

Na Mzidalfa Zaid

Vifaa hivyo vimekabidhiwa na Naibu Kamishna wa zima moto DCF Bashiri Madhebi mkuu wa kitengo cha maokozi makao makuu ya jeshi la zima moto na uokoaji, amesema vifaa hivyo ni mwendelezo wa jitihada zinazofanywa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Afisa habari wa jeshi la zima moto na uokoaji  mkoa wa Manyara Chande Abdallah , amesema vifaa walivyopokea ni pamoja na mitambo, vifaa vinavyotumika katika maokozi kwenye majengo marefu, kwenye maji na ajali za bara barani na vifaa hivyo vitasambazwa katika wilaya zote za mkoa wa Manyara.

sauti ya Afisa habari wa jeshi la zima moto na uokoaji  mkoa wa Manyara Chande Abdallah