FM Manyara

Madereva waonywa kuendesha kwa mwendo kasi Manyara

8 January 2026, 3:59 pm

Picha ya Afisa wa jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani kitengo cha elimu Sajenti Doto Aloyce

Madereva wa vyombo vya moto mkoani Manyara wametakiwa kuendelea kuchukua tahadhari  wanapokuwa katika barabara kuu zote kwa kufuata alama za usalama  barabarani ikiwemo kupunguza mwendo kasi ili kuepukana na ajali zisizotarajiwa.

Wito huo umetolewa na Afisa wa jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani kitengo cha elimu Sajenti Doto Aloyce alipozungummza na Fm Manyara amesema kwa sasa ajali zimepungua kutokana na elimu wanayoendelea kuitoa kupitia vyombo vya habari pamoja na mikusanyiko mingine ya watu.

Sauti ya Afisa wa jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani kitengo cha elimu Sajenti Doto Aloyce

Aidha Sajenti Doto amesema kwa mabasi ya masafa marefu yanayotembea zaidi ya masaa nane yanatakiwa kuwa na madereva wawili ambao watapeana muda wa kupumnzika ili waweze kuwafikisha salama abiria waliowabeba.

Sauti ya Afisa wa jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani kitengo cha elimu Sajenti Doto Aloyce

.