FM Manyara
FM Manyara
5 January 2026, 5:09 pm

Wananchi wilayani Babati mkoani Manyara wametakiwa kuchukua taadhari katika kipindi hiki ambacho mvua zinaendelea kunyesha ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea kutokana na mvua.
Na Mzidalfa Zaid
Taadhari hiyo imetolewa leo na Mkuu wa jeshi la zima moto na uokoaji wilaya ya Babati mkoani Manyara Emmanuel Kibona, wakati akiongea na fm Manyara ,amesema wananchi wanapaswa kuchukua taadhari kubwa katika madaraja yatakayosombwa na maji.
Aidha, Kibona amewataka wananchi kutoa taarifa kwa jeshi la zima moto na uokoaji kwa kupiga simu bure kwa namba 114 wanapokumbwa na majanga mbalimbali ikiwemo moto au kuzama maji ili jeshi hilo liweze kutoa msaada kwa uharaka zaidi.