FM Manyara
FM Manyara
19 December 2025, 8:58 pm

Mganga mkuu wa mkoa wa Manyara Dokta Andrew Method amewataka wakaguzi wanao hakiki ubora wa dawa za binadamu, mifugo na vifaa tiba kuhakikisha wanawafikia wananchi na kuwapati elimu juu ya matumizi sahihi ya dawa.
Na Mzidalfa Zaid
Dr Method amesema hayo leo alipokuwa mgeni rasmi katika mafunzo yaliyoandaliwa na Mamlaka ya dawa na vifaa tiba (TMDA) kanda ya kaskazini ambayo yamewakutanisha wakaguzi wanao hakiki ubora wa dawa za binadamu ,dawa za mifugo , vifaa tiba na vitenganishi katika halmashauri zote za mkoa wa Manyara.

Kwa upande wake Meneja wa Mamlaka ya dawa na vifaa tiba (TMDA) kanda ya kaskazini Proches Patrick amesema lengo la mafunzo hayo ni kuongeza ujuzi kwa watumishi hao ili wafanye kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa.
Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wameishukuru Mamlaka ya dawa na vifaa tiba (TMDA) kwa kutoa mafuzo hayo kwani wamejifunza mengi yatakayowasaidia katika utendaji wao wa kazi.
