FM Manyara
FM Manyara
17 December 2025, 4:57 pm

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen sendiga Amewataka wananchi wa Mkoa wa Manyara kuhifadhi chakula ili kuondokana na bar la njaa wakati wa Mabadiliko ya tabia ya Nchi.
Na Emmy Peter
Sendiga ameyasema hayo wakati wa ziara yake wilaya ya Mbulu mkoa wa Manyara alipokwa akisikiliza kero za wananchi wa wilaya hiyo na kuzitatua, amesema wananchi wanapaswa kutunza chakula kwakua mwaka huu hakuna mvua ya kutosha ambapo amesema ni jambo jema kila kaya Kuwa na utaratibu wakuhifadhi chakula kidogo kidogo.
Aidha, Sendiga amesema njaa ni adui wa maendeleo kwa wananchi hali inayo pelekea kushuka kwa utendaji kazi kwa jamii pamoja na kuzorota kwa uchumi wa kila mmoja pindi linapotokea bar la njaa.