FM Manyara
FM Manyara
28 November 2025, 10:12 pm

Wananchi mkoani Manyara wametakiwa kushiriki zoezi la usafi katika maeneo yanayowazunguka kama ulivyo utaratibu wa kufanya usafi kila jumamosi ya mwisho wa mwezi hapa nchini.
Na Mzidalfa Zaid
Afisa afya mkoa wa Manyara Suten Mwabulambo, amesema halmashauri zote mkoani humo zimejipanga kushiriki zoezi hilo la usafi ambapo litaanza saa kumi na mbili asubuhi hadi saa tatu asubuhi.
Aidha, amewataka wananchi kuendelea kutunza mazingira kwa kutotupa taka hovyo ili kuweka mazingira katika hali ya usafi.