FM Manyara

KAKUTE Project yawapatia majiko banifu na Sola Wananchi zaidi ya 500

22 November 2025, 10:47 am

Shirika lisilo la kiserikali  la  kakute Project kwa kushirikiana na shirika la maasai stove wamewafikia wananchi  zaidi ya 500 kwa kuwapatia majiko banifu, sola na elimu ya mjasiriamali katika wilaya za Monduli na Babati

Na Diana Dionis

Afisa mradi wa Shirika la kakuto Project Abdullaziz Rashid amesema hadi sasa wameshatoa elimu ya nishati safi, uhifadhi wa mazingira pamoja na elimu ya ujasiriamali.

Sauti ya Afisa mradi wa Shirika la kakuto Project Abdullaziz Rashid

Afisa mtendaji wa kata ya Mwada Rajabu Shaban, amelishukuru Shirika hilo kwa kuwafikia wananchi kwa lengo la kuwanufaisha.

sauti ya Afisa mtendaji wa kata ya Mwada Rajabu Shaban

Aidha, baadhi ya wanufaika wa mradi huo  Lucia Loomi pamoja na mwalimu Gabriel Nicodemus wameelezea jinsi walivyonufaika na mradi huo.

sauti ya wanufaika