FM Manyara
FM Manyara
29 October 2025, 10:49 am

Mkuu wa wilaya ya Kiteto Remidius Mwema, amesema hali ya usalama katika wilaya yake imeimarika katika vituo vyote vya kupigia kura na kuwataka wananchi kuendelea kujitokeza kupiga kura Ili wawachague viongozi wanaowataka.
Na Mzidalfa Zaid
Mwema amesema hayo wilayani Kiteto mkoani Manyara baada ya kushiriki zoezi la kupiga kura ya kumchagua Rais ,wabunge na madiwani katika kituo alichojiandikisha, ambapo amesema ulinzi umeimarishwa katika wilaya yake.
Kwa upande wake msimamizi wa uchaguzi Jimbo la kiteto Ally Kichuri amesema jumla ya vituo 560 katika Jimbo lake vinatumika Katika zoezi la upigaji kura.
Aidha, Wananchi wilayani kiteto mkoani Manyara wameendelea kujitokeza kupiga kura katika vituo mbalibali, ambapo wamesema wametimiza haki Yao msingi ya kikatiba.
Fm Manyara imetembelea vituo mbalibali vya kupigia kura katika wilaya ya Kiteto na kuzungumza na wananchi ambao wamejitokeza kupiga kura, wamesema hakuna changamoto yeyote ambayo imejitokeza kwani usalama upo wa kutosha.